April 13, 2016


Yanga imeitwanga Mwadui FC kwa mabao 2-1 na kubaki kiporo kimoja tu cha Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Lakini kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ anaamini Yanga inabebwa.

Julio amesema Yanga wanabebwa na hata beki wake aliyepewa kadi ya pili ya njano kuwa nyekundu hakustahili.

“Umeona tulivyocheza leo, nafikiri hawa Yanga wangewapa tu hilo kombe hata kabla ya ligi kwisha.

“Inaonekana wamelenga walipate, maana hata ucheza vipi hauwezi kuwafunga,” alisema Julio.

“Mimi ni msemakweli, watu wote wameona kama Yanga walibebwa na si jambo la kuiuanamichezo.”


Mwadui ilionyesha soka safi na la kuvutia, lakini makosa ya mwisho ya viungo na mabeki yake yalisababisha Haruna Niyonzima kuwamaliza kwa bao safi kabisa.

6 COMMENTS:

 1. Mbona coast waliwafunga!? Mbona mgambo na pridon walitoa droo!! Tatizo la makocha wa kibongo wanakuwa mashabiki badala ya kuongea kitaalamu!! Hakuna makocha nawakubali kama Mayanja na Major wa ndanda maana wanaongea kitaalamu na walipofanya kosa wanakiri

  ReplyDelete
 2. Swali la kujiuliza kwa nini YANGA IBEBWE?Ni timu ya tajiri gani?Au ni timu ya kampuni gani kusema labda pesa(rushwa) ndio inatumika kuibeba?Huwa haliniingii akilini hilo,Hivi hao marefa wote ni YANGA?Kama ni viongozi wako mawaziri/wabunge wanaoipenda YANGA na wapo wa SIMBA pia,au YANGA huwa hawana/hawapewi adhabu?
  Kadi za njano/nyekundu hata YANGA wanapewa sana.

  ReplyDelete
 3. Tatizo letu tumejaa ushabiki badala ya utaalamu wa michezo,aibu kwa kocha kama kihwelo kutoa maneno ya kipuuzi kama hayo kwani taifa linamtegemea halafu hataki kuheshimu kanuni za mchezo.Mwenzie Mayanja alipofungwa alisema wachezaji wake wamemuangusha sasa yeye jamhuri analeta unazi badala ya utaalamu,eti naye kocha!

  ReplyDelete
 4. Mi nashindwaga kumuelewa mtu asiye kubali ukweli. Kuna wakati unabidi ukubali kuwa mtu ulizidiwa ufundi sasa ndio kama huyu Julio kwanini asikubali kuwa walishindwa kumiliki mipira wakawa wanapoteza muda wanavyo jua wao... Kisha wenzao kwa uchu wa ushindi wakaweza kupata bao.

  Tatizo timu zetu ndogo ni hazina mipango, zipo tu ili mradi ziwe kwenye ligi kuu ila cha kusema kuwa labda zishindane kisoka ziweze kutoka huku walipo.

  Wanatakiwa wabafilike!... Sio kila siku kung'ang'ania kuwa timu kubwa zina bebwa

  ReplyDelete
  Replies
  1. Huyu Julio ni shabiki wa simba damu, ndo maana akifungwa na YANGA anasema kaonewa, akifungwa na simba anachukulia poa tu hasemi chochote. Wakuonee we julio una nini? Huo sio weledi wa ufundishaji soka, ni kuua soka letu ndo maana makocha wa bongo hampati timu za nje.

   Delete
 5. Mwacheni julio aseme ukweli, yanga wanabebwa sana. Ila mbeleko yao itaenda kukatikia misri.

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV