April 18, 2016Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameitisha Azam FC akidai inakwenda kwenye uwanja wa machinjio wa Mwadui na lazima wawatoe kwenye michuano ya FA ili wapate nafasi ya kuwakilisha nchi kimataifa.

Mwadui itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Mwadui katika mtanange mkali unaosubiriwa kwa hamu utakaochezwa Aprili 24, mwaka huu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Julio amesema lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanaitoa Azam kwenye michuano hiyo ili waweze kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kimataifa hapo mwakani.

“Tunajua tutakutana na Azam timu ambayo ni kubwa na yenyewe itakuwa na uhitaji mkubwa wa kushinda na kutwaa nafasi hiyo, lakini hatuhofii kwa kuwa tunajua wanakuja kucheza katika uwanja wa nyumbani, lazima tuwaondoe.

“Tutapambana hadi tone la mwisho katika michuano hiyo ili niweze kupata nafasi ya uwakilishi kimataifa, kwani nakiamini kikosi changu kipo vizuri na kina ushindani zaidi kwenye ligi,” alisema Julio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV