April 28, 2016


Beki wa Yanga, Juma  Abdul amekuwa gumzo katika mitandao mbalimbali ya nchini Misri.

Mitandao ambayo inawahusisha mashabiki wa Al Ahly ambao wanaeleza kushangazwa na namna Yanga ilivyokuwa ngumu licha ya kufungwa kwa mabao 2-1 katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Lakini wengi wanaonekana kufurahishwa na Abdul ambaye licha ya kukaba sana lakini alisababisha bao la Yanga baada ya kutoa krosi safi na Donald Ngoma akamalizia kwa umahiri mkubwa.

Wengi walimsifia Ngoma kwa kumalizia vizuri lakini wakasisitiza, sifa ziende kwa beki huyo aliyecheza soka la kuvutia huku wakitania kwamba anaweza kucheza Al Ahly.


Katika mtandao wa mashabiki wa Al Ahly maarufu kama Ultras Ahlyway, nao walimsifia beki huyo lakini mara nyingi zaidi wanaipongeza timu yao kwa mchezo mzuri.

Beki huyo wa kulia wa Yanga, alitoa pasi iliyozaa bao la kusawazisha wakati Yanga ikiwa nyuma kwa bao moja. Alifanya hivyo baada ya kumtoka beki wa Ahly kwa umakini mkubwa.

Yanga ilipoteza mechi hiyo kw akufungwa mabao 2-1 na kung'olewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2.

2 COMMENTS:

  1. Goli la Tambwe Azam TV tuonyesheni picha iliyopigwa na kamera ya nyuma ya goli tuondoe utata au na nyinyi ni jipu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hamna kitu,wangekuwa wameshaonyesha.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic