April 2, 2016


Kesho Jumapili, Kagera Sugar itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kupambana zaidi na siyo kinyonge kama inavyofikiriwa ili wasishuke daraja.

Katika Ligi Kuu Bara, Kagera Sugar ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 25, ambazo ni tofauti ya pointi sita tu na zile za Coastal Union inayoshika mkia ikiwa na pointi 19.

Yanga yenyewe ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 50 na kocha wake, Hans van Der Pluijm amesema kikosi chake kipo vizuri kushinda mechi hiyo kutetea ubingwa wao.

Kocha wa Kagera Sugar, Adolf Rishard amesema: “Yanga isitegemee mteremko katika mechi hiyo, naona wamejipanga kuhakikisha wanashinda ili wajiweKe katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa.

“Sisi hatukubali kufungwa kirahisi, tutapambana kuepukana na balaa la kushuka daraja maana hali si nzuri kwetu na ligi haijakaa vizuri.


“Tunaijua Yanga ni timu bora yenye wachezaji wengi wazuri wengine kutoka nje ya nchi, lakini na sisi tutapambana kwa uwezo wetu ili tupate pointi.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV