Kiungo wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza ni kati ya viungo wanaoheshimika sana nchini Rwanda.
MIGI AKIWA KAZINI AZAM FC... |
Mugiraneza ambaye alikuwa APR ya Rwanda kabla ya kutua Azam FC ni mmoja wa viungo wakabaji bora katika ukanda wa Afrika Mashariki na kivutio kwa Wanyarwanda wengi kutokana na tabia yake ya “mtu mwenye nidhamu”.
Taarifa zinaeleza Mugiraneza hatumii kilevi chochote, pia si mtu wa mambo mengi na ana heshima ya juu kwenye kazi yake.
Pia kwa wachezaji wanaotokea katika nchi ndogo ya Rwanda ni kati ya wenye mafanikio kwani anamiliki gari la kifahati aina ya Mercedez Benz ya milango miwili, hili hulitumia kwa matembezi yake.
Pia anamiliki gari aina ya Toyota Coaster inayofanya kazi ya kusafirisha abiria tokea Kigali hadi Kimironko kupitia Uwanja wa Amahoro hadi Nyabugogo, ingawa yeye amekuwa akifanya siri kubwa kwa kuwa si mtu wa majigambo na hapendi kuonekana ni mtu mwenye nazo kama ambavyo wangependa wengine wenye tabia za "mnaniona."
Kama hiyo haitoshi, kiungo huyo anamiliki nyumba tatu, awali alikuwa na mbili na siku chache zilizopita michache imepita amenunua ya tatu katika enero la Bugesera nje kidogo ya jiji la Kigali. Hivyo unaweza kusema amejitosheleza na sasa anaendelea kusaka maisha hapa nchini Tanzania.
Haruna Niyonzima na Mugiraneza maarufu kama Migi walikutana katika mashindano ya kukuza vijana, Haruna akikipiga katika timu yake ya Etiencel kutoka katika mkoa wa Gisenyi aliozaliwa na Migi kutoka Kigali akichezea timu ya “kitaani” kwao ya Jenesi.
0 COMMENTS:
Post a Comment