April 9, 2016


Straika wa zamani wa Nigeria na Arsenal, Nwankwo Kanu jana Ijumaa alikabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Majimatitu, Mbagala, Dar.

Kanu ambaye ni Balozi wa Startimes Afrika, yupo nchini katika ziara maalum na alifika shuleni hapo ambapo kuna kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum, kisha akakabidhi mchele, unga, magodoro, sabuni, runinga na king’amuzi cha Startimes.


Akizungumza baada ya kukabidhi vitu hivyo, Kanu alisema: “Nimefurahishwa kufika kituoni hapa, ninaahidi kushirikiana nanyi na kama kuna kitu hakitaenda sawa nitatatua tatizo hilo.”

Kanu yuko nchini akiwa ni balozi wa ving'amuzi wa StarTimes na tayari ametembelea sehemu mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV