April 1, 2016

AJIB (KULIA)...
Mshauri wa benchi la Ufundi la Taifa Stars na Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Abdallah ‘King’ Kibadeni amemwambia mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib kama akiongoza bidii ya ndani ya uwanja na kujitambua, basi atamfuata Mbwana Samatta barani Ulaya.

Samatta hivi karibuni alijiunga na KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya DR Congo.

Kibadeni amesema Ajib amekosa vitu vichache ambavyo kama akipewa maelekezo, basi atabadilika.

“Mchezaji bora kwenye timu, ni yule anayetoa mchango kwenye timu na siyo kitu kingine chochote, hivyo kutokana na mchango huo anaoutoa kwenye timu, basi ninampa uchezaji bora kwenye msimu huu.

“Ajib ni kati ya wachezaji wenye vipaji vya soka wanaohitajika kupewa matunzo mazuri kwa ajili ya faida ya taifa hapo baadaye na vijana wengine wanaochipukia.

“Ninaamini kama Ajib akijitambua na kutimiza wajibu wake kwa asilimia 90, basi njia ni nyeupe kwake ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya kama ilivyokuwa kwa Samatta,” alisema Kibadeni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV