April 1, 2016

MAYANJA

Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja amesisitiza wachezaji wake kuachana na matumizi ya vilevi pamoja na soda ili kulinda afya zao.

Mayanja ambaye anasifika kuwa ni mtu anayesimamia nidhamu, tangu atue kikosini hapo mwanzoni mwa mwaka huu ameweza kuirekebisha Simba kinidhamu huku akiwaweka kitimoto nyota wawili wa kikosi hicho, Hassan Isihaka na Abdi Banda kutokana na utovu wa nidhamu.

Mayanja alisema soda ina kemikali ambayo kiafya si nzuri, hivyo amewakataza wachezaji wake kutumia kinywaji hicho na badala yake wawe wanakunywa maji kwa wingi kwani ndiyo muhimu katika mwili wa binadamu.


“Sitaki nione mchezaji anakunywa soda na akibainika mmojawapo akifanya hivyo hatutamvumilia. Kila siku nawaambia wawe wanakunywa sana maji na kuachana na soda ambazo zina kemikali hatarishi kwa afya ya binadamu,” alisema Mayanja. 

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV