Kocha wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja amefunguka kuwa tangu beki wake na aliyekuwa nahodha wa kikosi, Hassan Isihaka arejee ndani ya timu hiyo ameweza kubadilika kwa kiasi kikubwa hasa kwenye upande wa nidhamu.
Isihaka alisimamishwa na uongozi wa timu hiyo kwa mwezi mmoja na kuwa nje ya kikosi hicho kutokana na utovu wa nidhamu ambao aliuonyesha kwa kocha huyo.
“Hivi ndivyo inatakiwa unajua ili mchezaji aweze kufanikiwa kwa urahisi ni lazima awe na nidhamu ya hali ya juu jambo ambalo utaona mimi nimekuwa nikilisimamia kwa ukaribu na nataka kila mchezaji aweze kulifuata.
“Tangu Isihaka kajiunga nasi tena ameweza kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kwa jambo hilo kwa hakika naweza kumpongeza na namtaka aweze kuendelea hivyo kwa kipindi chote,” alisema Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment