KIFARU |
Mtibwa Sugar wamesema mechi yao dhidi ya Azam FC ilikuwa nzuri lakini walipoteza kihalali.
Mtibwa Sugar ikiwa nyumbani kwao Manungu, ilipoteza kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema Azam FC, walitumia nafasi walizozipata.
“Wenzetu walitumia nafasi chache walizopata. Lakini tunaamini tuna nafasi ya kujirekebisha dhidi ya Yanga. Hatuwezi kuwa watu wa kukubali kufungwa tu ndugu yangu Saleh, Mtibwa ndiyo kiboko ya Yanga.
“Tunakuja kucheza na Yanga Jumamosi. Lakini kazi itakuwa ngumu kwao na kwetu pia. Wajue tu hakutakuwa mteremko,” alisema Kifaru.
Mtibwa Sugar itaivaa Mtibwa Sugar katika mechi ya kiporo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment