April 6, 2016


Ndanda FC imeonyesha si laini baada ya kuilazimisha sare ya mabao 2-2 Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Azam FC ilitangulia kufunga mabao mawili kupitia Ramadhani Singano ‘Messi’ na Didier Kavumbagu na kuonyesha dalili ingeweza kushinda hata mabao manne.

Lakini juhudi hizo zikakwama baada ya Atupele Green kusawazisha kwa bao la penalti kabla ya Hemed Msumi aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la pili.

“kuchacha” kwa kiporo hicho kuinaifanya Azam FC kufikisha pointi 54 baada ya mechi 23, hivyo inalazimika kushinda mechi yake ya 24 ili kuifikia Simba iliyo kileleni ikiwa na pointi 57.

Sare hiyo imeifanya Yanga isogee katika nafasi ya pili juu ya Yanga yenye pointi 53, lakini ina mechi moja nyuma kwa Azam.


4 COMMENTS:

 1. Si kweli,kwa matokeo hayo Azam imefikisha point 52,weka kumbukumbu zako sawa.

  ReplyDelete
 2. Mlizidi kuwasifia, si walisema mwanza mvua na uwanja mbovu!? Vipi chamazi!?

  ReplyDelete
 3. Meneja wao alisema wakimaliza viporo vyao Simba watarudi kwenye nafasi yao ya tatu walioizoea

  ReplyDelete
 4. Meneja wao alisema wakimaliza viporo vyao Simba watarudi kwenye nafasi yao ya tatu walioizoea

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV