April 6, 2016KATANI...
Mbunge wa Tandahimba kupitia Chama cha Wananchi (Cuf), Katani Ahmad Katani ametoa kitita cha Sh 500,000 kwa wachezaji wa Ndanda FC baada ya kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam FC, leo.

Ndanda FC imeonyesha si laini baada ya kuilazimisha sare ya mabao 2-2 Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Katani amesema amefurahishwa na Ndanda na pia kuahidi kutoa Sh milioni moja kwa kila mechi ambayo Ndanda watashinda.

“Pia nitanunua kila bao watakalofunga kwenye mechi zao, Ndanda ni timu ya mkoa wa Mtwara ambako ninatokea. 

Ninafanya hivi kuwahamasisha vijana ili wapambane zaidi,” alisema Katani.


Ndanda ilionyesha soka la kuvutia katika kipindi cha pili wakati wa mechi yao dhidi ya Azam FC leo na kusawazisha mabao yote mawili baada ya wenyeji wao kutangulia kwa kuwafunga mabao mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV