Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kitaendelea kesho Jumamosi saa 3 asubuhi katika ofisi za TFF zilizopo Karume, na maamuzi yake yatatangazwa saa 7 mchana.
Tayari baadhi ya wajumbe waliotakiwa kuja wamesema hawatahudhuria kikao hicho. Kwa kuwa kile cha awali hawakuelezwa kwa nini kiliahirishwa na wana kazi zao nyingine za kuendesha maisha.
Kamati inakutana kwa ajili ya kumalizia shauri la upangaji wa matokeo Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League) kundi C inayozihusisha timu za Geita Gold, JKT Kanembwa, JKT Oljoro na Polisi Tabora.
Viongozi watakaohojiwa na Kamati ya Nidhamu ni, Yusuf Kitumbo (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tabora), Fateh Remtullah (Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tabaora), viongozi wa benchi la ufundi Polisi Tabora, Mrisho Selemani, Boniface Komba, Bernard Rabiamu.
Kamati pia itawahoji Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita, Salum Kurunge na mwenyekiti wa Klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita.
0 COMMENTS:
Post a Comment