April 26, 2016


Aliyewahi kuwa Kocha wa Makipa wa Simba, Iddi Salim, mambo yanazidi kumyookea Ulaya baada ya timu yake kushinda mechi mbili mfululizo.

Timu yake ya MFK Topolcany inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Slovakia imeendelea kufanya vizuri baada ya juzi kushinda tena kwa bao 1-0.“Kweli ni jambo zuri, timu inaendelea kufanya vizuri. Baada ya ushindi wa jana tunaendelea kujiandaa zaidi,” alisema kocha huyo raia wa Kenya ambaye pia ni kocha wa makipa katika kikosi cha MFK Topolcany.

Kuhusiana na mazingira, Iddi amesema awali alipata shida kidogo kuzoea lakini haikuwa sana.

“Sasa naendelea vizuri kabisa na mambo yanakwenda vizuri. Napata ushirikiano mzuri hapa na kazi inakwenda vizuri kabisa.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV