April 1, 2016Wakati Yanga ikishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda FC katika mechi ya Kombe la Shirikisho, siku moja kabla Al Ahly ilikuwa imeanza kuonyesha ina uwezo wa kushinda pia katika mechi ya Kombe la Misri kwa kuichapa Derot ya daraja la kwanza nchini humo kwa mabao 3-0.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria ilishuhudia mabao kutoka kwa Fathy Ahmed dakika ya 11 kisha Sheikh Ahmed katupia mawili dakika ya 61 na 64.

Kutokana na matokeo hayo Al Ahly imesonga mbele sasa itavaana na Haras El Hodood katika hatua inayofuata Aprili 28, mwaka huu. 


Aidha, Al Ahly inatarajiwa kucheza dhidi ya El-Shorta keshokutwa Jumapili katika Ligi Kuu ya Misri, ambapo Al Ahly ni kinara wa ligi hiyo huku El-Shorta ikishika nafasi ya 16 katika msimamo wenye timu 18.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV