April 15, 2016


Liverpool imefuzu kucheza nusu fainali ya Europa Cup huku ikilazimisha kusawazisha mabao matatu kabla ya kufunga la nne.

Ikiwa nyumbani, Liverpool ilifungwa mabao 2-0 yaliyodumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza, kabla ya kuanza kusawazisha katika kipindi cha pili.

Lakini hata baada ya kupata moja lililofungwa na Divok Origi katika dakika ya 48, Marco Reus akaongeza jingine yaani la tatu kwa Dortmund katika dakika ya 57.

Baada ya hapo, Liverpool wakakaa na kuanza kurudisha bao moja baada ya jingine wakianza na dakika ya 66 kupitia Mbrazili, Phillippe Coutiho aliyepiga shuti kali kimo cha mbuzi.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ambaye ni kocha wa zamani wa Dortmund, ndiye aliyeonekana mwenye furaha zaidi huenda kupita mtu mwingine yoyote.

Beki Mamadou Sakho akaongeza bao la kichwa katika dakika ya 78 kabla ya beki mwingine wa kati, Dejan Lovren kumaliza kazi katika dakika ya 90 akipiga kichwa krosi safi ya James Milner aliyeng’ara katika mechi ya leo.


Liverpool wameonyesha kuwa kweli “U ll Never Walk Alone” kutokana na walivyojituma tokea mwanzo hadi mwisho wa mechi.

Liverpool wanavuka kwa jumla ya mabao 5-4 kwa kuwa katika mechi ya kwanza nchini Ujerumani, walilazimisha sare ya bvao 1-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV