Na Saleh Ally
Yanga ina kazi kubwa ya kurudisha imani kwa mashabiki wake hasa katika mechi zake inazocheza nyumbani.
Mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, ndiyo mechi ambazo Yanga inaonekana haijacheza vizuri sana nyumbani. Leo Yanga inakutana na wababe wa Afrika, Al Ahly ya Misri.
Mechi ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Circle de Joachim ya Mauritius ambayo Yanga ilishinda kwa mabao 2-0.
Lakini kulikuwa na makosa mengi yaliyoifanya Yanga kushindwa kufunga na kuibuka na ushindi huo.
Pamoja na hivyo, Yanga ilishindwa kutumia nafasi nyingi ilizozipata. Lakini mechi nyingine dhidi ya APR, mechi ikaisha kwa sare ya bao 1-1.
Sare hiyo dhidi ya APR, mashabiki waliomba mpira uishe hasa kwa kuwa Yanga iliziddiwa sana.
Leo inakutana na Al Ahly ya Misri, moja ya timu kubwa barani Afrika lakini ikiwa na vijana wengi wenye uwezo kama Ramadan Sobhy.
Katika mechi mbili zilizopita, Yanga ilianzia ugenini, ikashinda mechi zote kwa mabao 1-0 na 2-1. Lakini nyumbani ikashinda 2-0 na sare ya 1-1 lakini kiwango hakikuwa kizuri.
Inakutana na Ahly kwa kuanzia nyumbani, utaona game plan imebadilika na Yanga lazima wajue wanatakiwa kumaliza mchezo DAr es Salaam, ili Misri wakale mkia.
Hivyo ni lazima wabadilike, wabadili mchezo, wafunge mabao na kuhakikisha wanaipa presha kubwa Al Ahly katika mechi ya marudiano.
Uhakika wa Yanga itatengeneza nafasi katika mechi hiyo, upo. Swali watazitumia nafasi hizo? Jibu ni chaguo lao, wazitumie wawe katika nafasi nzuri mechi ya marudiano, au waziache kazi ngumu iwe kwao.
Tusubiri mechi
0 COMMENTS:
Post a Comment