April 9, 2016




MPIRA UMEKWISHAAAAAAA....Evouma anajirusha na kuanguka ndani ya eneo la hatari lakini wamuzi kutoka Ivory Coast anamuambia amka twende
Katika dakika 2 za nyongeza, Yanga wanagongeana vizuri lakini umaliziaji unakuwa ni uleule
DAKIKA 4+ ZA NYONGEZA
Dk 87 hadi 89 timu zaidi zinagongeana pasi ambazo hazina manufaa kwani hakuna hata moja iliyopiga shuti lililolenga lango
Dk 86, inaonekana Ahly wameridhika na walichokitaka, lakini wanalazimika kuwa makini kwa kuwa Ahly wanaweza "kuwaotea" na kuwamaliza
SUB 85 upande wa Ahly, wanafanya mabadiliko ya mwisho Zacharia anatoka na nafasi yake inachukuliwa na rais wa Gabon, Malick Evouma


Dk 84, kipa Dida anamzoa beki wake Yondani wakati akiokoa mpira, lakini beki huyo anainua
Dk 82, Ngoma anageuka katikati ya mabeki watatu wa Ahly, lakini shuti lake linakwenda nje
SUB Dk 81, Deogratius Munish 'Dida' anaingia kuchukua nafasi ya Barthez ambaye baada ya kutibiwa amechukuliwa na kuingizwa kwenye gari la wagonjwa

Dk 74 hadi 76, Yanga wanaitumia kwa kugongeana, lakini kama ilivyo kawaida wanakwenda kumalizia kwa shuti dhaifu kabisa la Haji Mwinyi. Kipa Barthez yuko chini baada ya kuumia ubavuni, anatibiwa

Dk 73, Ahly wanafanya shambulizi jingine kali, lakini Bossou anaingia na kuosha mpira 'kindava'

SUB Dk 73 upande wa Ahly Hossan Ahour anaingia nafasi ya Hossan Hgally ambaye ni nahodha

hadi Dk 60 na 71, Yanga wanaonekana kuchangamka hasa katikati ya uwanja, wanagongeana vizuri lakini mipango ya mwisho katika umaliziaji inaonekana kutokuwa na nguvu
SUB Dk 68 Ahly wanamtoa Subh anaingia Waridi Suleyman
Yanga nao wanamtoa Tambwe na kumuingiza Msuva

Yanga nao wa
Dk 66, Ngoma anamchambua nahodha na Ahly na kuingia vizuri kabisa lakini mabeki wa Ahly wanaokoa na kuwa kona. Inachongwa  lakini haina madhara
Dk 66, hatari kwenye lango la Yanga lakini mabeki wa Yanga wanaokoa
Dk 65 bado mpira umepooza, Ahly wanaonekana wamewa "win" Yanga, kwani hawajafanya shambulizi kali katika kipindi cha pili huku wao wakionekana kufanya wanachotaka
SUB Dk 62, Geofrey Mwashiuya anaingia kuchukua nafasi ya Boubacar
Dk 61, Yanga wanaonekana kupoteza mipira mingi zaidi huku kiungo chao hasa cha ukabaji kinaonekana kutokuwa na uhakika 
Dk 59 anapiga mpira huo wa Kamusoko lakini anabutua juuuuuu...!!
Dk 58, Boubacary alikuwa akijaribu kuwatoka mabeki wa Ahly anaangushwa na kuwa faulo nje ya 18

Dk 56, Kaseke anampa Kamusoko pasi nzuri kabisa lakini anapiga mpira juuu. Hakuwa makini wakati anajiandaa kupiga mpira huo...


KADI Dk 54, Telela analambwa kadi ya njano kwa kumuangisha Abdallah Said. Bado Ahly wanaonekana kumiliki mpira zaidi
Dk 52, bado inaonekana hakuna shambulizi kubwa ambalo wamefanya Yanga katika kipindi hiki ukilinganisha na Al Ahly
Dk 49, bado Ahly wanaonekana kuwa bora kwa kujiamini zaidi huku Yanga wakionekana bado na hofu baada ya kupoteza mpira kila mara baada ya pasi mbili, tatu

DK 47, Ahly wanaonekana kuuthibiti mpira zaidi zaidi ya Yanga, huku Yanga wakipata mpira wanaipoteza mapema jambo ambalo si sahihi kwao walio nyumbani
Dk 46, Zacharia anamchambua Mwinyi na kupiga shuti linalogonga mwamba, ilikuwa hatari kwelikweli
MAPUMZIKO
DAKIKA 1+ YA NYONGEZA 
Dk 41 hadi 45, bado inaonekana Ahly kuwazidi ujanja Yanga, wanamiliki mpira katika eneo lao au kucheza taratibu

Dk 38 hadi 40, Ahly wanamiliki mpira muda wote lakini wanaonekana "kununua" muda kwani wanajua kubaki na mpira ndiyo ulinzi wao
Dk 37, Ngoma anawahadaa mabeki wa Ahly na kupiga shuti lakini kipa Akram yuko makini anadaka vizuri kabisa
Dk 34, hadi sasa Yanga wamefanya madhambi mara 5 na Ahly mara 4

KADI Dk 33, Kipa Akram analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda. Hii ni kadi ya kwanza katika mechi hii
Dk 32, Yanga wanafanya shambulizi jingine safi kabisa, lakini Telela anashindwa kumalizia mpira wa mwisho, goal kick

Dk 28 hadi 30, Yanga wanaotea mara mbili kupitia Yondani aliyepanda na Ngoma. Hali inayoonyesha inabidi wajipange kuutegua mtego huo
Dk 27, Said anamtoka Bossou na kupiga shuti la 'akili' lakini mpira unatoka kidogo nje ya lango la Yanga.
Yanga lazima wawe makini kwa kuwa kadiri muda unavyokwenda, inaonekana Ahly ndiyo wanauthibiti zaidi mchezo

Dk 23 hadi 26, mpira unachezwa katikati zaidi na ilivyo ni opening game, kwani mashambulizi ni kwa zamu
Dk 22, Yanga wanafanya shambulizi kubwa, krosi nyingine safi ya Boubacar lakini  anaokoa, mpira unamkuta Ngoma anapiga shuti dhaifu, kipa Shariff Akram anadaka kwa ulainiii
Dk 21, Gamal anapiga kichwa safi akiunganisha kona lakini mpira unatoka nje kidogo. KIpa Mustapha anaonekana kukasirishwa na walinzi

GOOOOOOOOO Dk 19, krosi safi sana ya Boubacary, beki Ahmed Said wa Al Ahly anautumbukiza mpira wavuni yeye mwenyewe...
Dk 16, Yanga wanagongeana vizuri, Kamusoko anampa pasi nzuri Abdul anapiga shuti kali lakini mpira unamgonga beki na kutoka nje, kona. Inachongwa na Boubacary lakini ni kona butuuu

Dk 12 hadi 14, Yanga wanaonekana kuchangamka lakini safu ya ulinzi ya Ahly iko makini sana na wamejaza watu zaidi ya watano GOOOOOOOOOO Dk 11, Amri Gamal anaipatia Yanga bao kwa kichwa baada ya kupiga mpira wa kichwa kutokana na faulo iliyowachanganya mabeki wa Yanga waliodhani angepiga shuti...

DK 10, Bossou anafanya madhambi karibu kabisa na lango la Yanga, faulo.
Dk 5, Juma Abdul anapiga mpira wa adhabu, shuti kali lakini linaishia mikononi mwa kipa

Dk 3, Al Ahly wanafanya shambulizi la kwanza lakini Yanga wanakuwa wepesi kung'amua mbinu zao
Dk 1, Ngoma anawatoka mabeki wa Ahly, lakini kabla hajapiga wanaokoa na kuwa kona, inapigwa na Boubacary, anaigonga Tambwe unatoka na kuwa goal Kick.

Mechi ndiyo imeanza na kila timu inaonekana iko makini.



KIKOSI CHA YANGA:
1. Ally Mustapha
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Thabani Kamusoko
7. Deus Kaseke
8. Salum Telela
9. Amissi Tambwe
10. Donald Ngoma
11. Yousouf Boubacary

BENCHI:
Deo Munishi
Oscar Joshua
Pato Ngonyani
Geofrey Mwahiuya
Simon Msuva
Paul Nonga



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic