WAPIGA BAO LA KUSAWAZISHA DAKIKA YA 95
Katika kile kinachoonekana kweli Leicester City ni wabishi na wamepania kuweka historia ya kuutwaa ubingwa wa Premier League kwa mara ya kwanza, wamelazimika kuswazisha bao dakika za majeruhi na mchezo wao dhidi ya West Ham United kumalizika kwa mabao 2-2.
Mchezo baina ya timu hizo ulikuwa ni sawa na ngoma siyo ya kitoto kutokana na timu zote mbili kupambana kwa nguvu zote kuanzia dakika ya kwanza.
Jamie Vardy ndiye alikuwa wa kwanza kucheka na nyavu katika dakika ya 18, lakini dakika ya 28 akapata kadi ya njano kisha dakika ya 56 akapata kadi ya pili ya njano kwa kujirusha katika eneo lwa West Ham.
Vardy alipinga tukio hilo kwa kulalamika kuwa alichezewa faulo lakini mwamuzi alishikilia msimamo wake na ndipo akakubali kutoka.
Dakika ya 84, Andy Carroll aliisawazishia bao West Ham kwa penalti kisha Aaron Cresswell kuongeza la pili dakika mbili baadaye.
Ikionekana kama vinara hao wa Premier wamekubali kichapo, dakika ya 90, Leicester City walipata penalti na ndipo Jose Leonardo Ulloa akatupia wavuni na kufanya matokeo kusomeka 2-2.
Licha ya matokeo hayo, mchezo huo ulitawaliwa na matukio mengine yakiwemo ya ubabe na wachezaji kutumia nguvu kama ilivyo kawaida ya ligi hiyo.
Leicester wameendelea kubaki kileleni wakiwa na pointi 73 wakifuatiwa na Tottenham wenye pointi 65.
Vardy akifunga bao la kwanza la Leicester |
Mchezo baina ya timu hizo ulikuwa ni sawa na ngoma siyo ya kitoto kutokana na timu zote mbili kupambana kwa nguvu zote kuanzia dakika ya kwanza.
Kipa wa Leicester, Schmeichel akishangilia baada ya timu yake kufunga. |
Vardy baada ya kupewa kadi nyekundu |
Claudio Ranieri akimfariji mchezaji wake, Vardy aliyetolewa kwa kadi nyekundu. |
Vardy alipinga tukio hilo kwa kulalamika kuwa alichezewa faulo lakini mwamuzi alishikilia msimamo wake na ndipo akakubali kutoka.
Dakika ya 84, Andy Carroll aliisawazishia bao West Ham kwa penalti kisha Aaron Cresswell kuongeza la pili dakika mbili baadaye.
Beki wa Leicester, Robert Huth akimfanyia ubabe Kouyate wa West Ham. |
Licha ya matokeo hayo, mchezo huo ulitawaliwa na matukio mengine yakiwemo ya ubabe na wachezaji kutumia nguvu kama ilivyo kawaida ya ligi hiyo.
Leonardo Ulloa akishangilia baada ya kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya 95. |
0 COMMENTS:
Post a Comment