April 17, 2016

John Tegete
Muda mfupi baada ya timu yake kuifunga Simba bao 1-0, Kocha wa Toto Africans, John Tegete amesema kuwa moja ya siri ambayo ilichangia timu yake kupata ushindi ni kitendo cha kuwazidi nguvu wachezaji wa Simba katika mchezo huo.

Toto imeifunga Simba bao 1-0 katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kupunguza kasi ya Simba katika mbio za kuwania ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya kupita zaidi ya misimu mitatu.

Tegete amesema kuwa kazi ambayo aliwatuma vijana wake waende wakaifanye katika mchezo huo waliifanya kwa usahihi na pia waliwazidi nguvu wapinzani wao uwanjani ndiyo maana wakajikuta wanapotezana muda fulani.

“Simba ni wazuri lakini walizidiwa nguvu na wachezaji wangu, yaani ile ya kukutana mtu na mtu ndiyo ambayo iliwaponza, nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi nzuri,” alisema Tegete.

Upande wa  Kocha wa Makipa wa Simba, Adam Abdallah alisema kupoteza mchezo ni jambo la kawaida kutoka katika soka, hivyo watajipanga kwa ajili ya mchezo ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic