April 23, 2016


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza Mei 14, 2016 kuwa tarehe ya kuanza kwa Ligi ya Mabingwa wa mikoa (RCL) itakayozishirkisha bingwa wa kila mkoa kutoka katika mikoa 27 nchini.

Ligi hiyo ya mabingwa wa mikoa itachezwa katika vituo vine nchini, ambapo mshindi wa kila kundi atapanda moja kwa moja ligi daraja la pili (SDL) na mshindi wa pili mwenye matokeo mazuri kutoka kundi A, B na C.

Kundi A kituo cha (Njombe) kutakua na mabingwa wa mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Dar es salaam 3, Morogoro, Kundi B kituo cha (Morogoro) kitakua na mabingwa wa mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi, Dar es salaam 1, Dar es salaam 2, Tanga, na Singida.


Kundi C kituo cha (Singida) kitakua na mabingwa wa mikoa ya Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Tabora, Kagera, Manyara, na Njombe, huku kundi D kituo cha (Kagera) kikiwa mabingwa wa mikao ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara na Kigoma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic