April 24, 2016

Adeyum analambwa kadi nyekundu

Tambwe anaifungia Yanga bao la pili kwa mkono
DK 90+7 MPIRA UMEKWISHAA NA SASA ZINAONGEZWA DAKIKA 30
Yanga wanajitahidi kugongeana na mpira wa krosi unamkuta Tambwe lakini kipa anaudaka

(MWADUI COMPLEX, MWADUI 1-2 AZAM FC, MCHA NDIYE ANAFUNGA NA MECHI INAENDELEA DAKIKA 30 ZA NYONGEZA)
DK 90+6 Yanga wanafanya shambulizi kali lakini mpira unaokolewa na kumgonga Tambwe, goal kick
KADI Dk 90+3, Cannavaro analambwa kadi ya njano
Dk 90+3 Sabo anapiga shuti kali lakini linapita kando ya lango la Yanga
DAKIKA 7 ZA NYONGEZA
Dk 90, Wambura anapiga shuti kali sana na Dida anafanya kazi ya ziada. Ilikuwa ni hatariiiiii
Dk 89, Mahadhi Juma anamtoka Oscar Joshua lakini anashindwa kumalizia vizuri nafasi hiyo, Yanga wanaokoa
KADI 87 Adeyum analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Niyonzima
Dk 86, Tambwe anaruka na kupiga kichwa safi kabisa lakini kipa Coastal anadaka kwa umahiri akiajiamini na kuanzisha mpira haraka

(MWADUI COMPLEX MECHI IMEISHA NA MWADUI 1-1 AZAM FC, WANASUBIRI DAKIKA 30 ZIONGEZWE)
Dk 84 Adeyum anapiga shuti kali sana, lakini Dida anaokoa kwa juhudi kubwa
Dk 83 Shiboli anapiga shuti kali lakini Dida anaokoa vizuri
SUB Dk 81 Yanga inamtoa Ngoma mfungaji wa bao lao na nafasi yake inachukuliwa na Amissi Tambwe
SUB Dk 80, Ismail anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Shiboli
Dk 75 hadi 78 mpira unaonekana kupooza kama kila timu ikicheza kwa kuvizia
SUB Dk 74, Yanga wanamtoa Yondani na kumuingiza Malimi Busungu, mchezaji wa zamani wa Coastal Union na Mgambo
(TAARIFA KUTOKA MWADUI COMPLEX ZINAELEZA, MWADUI FC WAMEFANIKIWA KUSAWAZISHA BAO SASA NI 1-1)
Dk 70, Adeyum anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa shuti wa Kamusoko. Hata hivyo mwamuzi anasema aliotea
DK 67, wachezaji Coastala Union wanarejea uwanjani na mpira unaendelea huku Coastal wakionekana kuumikili tena
Dk 66 mpira bado umesimama, bado kuna mzozo hapa na pale
Dk 63 mpira unasimama baada ya mashabiki wa Coastal Union kuanza kufanya vurugu huku wakionekana kumtupia vitu mwamuzi msaidizi Charles Simon
GOOOOOOOOO Dk 60 Ngoma anaisawazishia Yanga baada ya mabeki wa Coastal Union kusimama wakidhani alikuwa ameotea
Dk 55 hadi 58, Coastal bado wanaendelea kutawala zaidi hasa katikati ya uwanja na Yanga wanaonekana kuchanganyikiwa wakipteza pasi nyingi

GOOOOOOOO Dk 54 Yossiuf Sabo anaifungia Coastal Union bao kwa shuti kali la chinichini baada ya Ayoub Semtawa kuwachambua mabeki wawili wa Yanga
Dk 52, Bossou analazimika kufanya kazi ya ziada na kutoa mpira unaokuwa kona. Juma Mahadhi alikuwa anakwenda kasi kwenye lango la Yanga. Inachongwa kona safi lakini Cannavaro anaokoa kwa kichwa

Dk 47 na 48, Coastal Union wanapata kocha pacha, yaani kona mbili mfululizo baada ya kufanya shambulizi kali kupitia Ismail na Juma Mahadhi ambaye anaonekana kumpa wakati mgumu Kelvin Yondani
SUB Dk 46  Yanga wanamuingiza Msuva kuchukua nafasi ya Yossouf
MAPUMZIKO
-Kaseke anapata nafasi nzuri anaingia lakini anashindwa kuwa makini, anashindwa kutoa pasi nzuri kwa Ngoma
-Niyonzima anapiga mpira wa adhabu unatoka kidogo juu ya lango la Yanga
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 44 Hamad Juma anamkwatua Yossouf, yuko chini anapatiwa matibabu, Yanga wanasubiri kupiga faulo hiyo
(MWADUI COMPLEX SASA NI MAPUMZIKO, MWADUI 0-1 AZAM)
Dk 43, Bossou na Cannavaro wanaonekana wanataka kufanya mzaha katika safu ya ulinzi, hata hivyo Coastal wanakuwa si wepesi na hiyo ndiyo nafuu kwa Yanga
Dk 42, kinachoonekana Coastal Union ndiyo wameutawala zaidi mchezo na mashambulizi yao yanakuwa makali ukilinganisha na yale ya Yanga
Dk 41 Yossouf anaingiza krosi nzuri na Juma Abdul anauwahi lakini mabeki wa Coastal wanamuwahi na kuondosha hatari
Dk 39, Beki Bossou wa Yanga anaokoa mpira kwa kupiga kichwa cha nyuma, inakuwa kona lakini Coastal wanashindwa kufanya lolote kuzitumia kona hizo
 Dk 35 hadi 38, Awadhi Juma na Godfrey Wambura wanaonekana kutawala katika sehemu ya kiungo na kuwapa wakati mgumu viungo Haruna Niyonzoma na Kamusoko
Dk 34 Joshua anapiga mpira ndani ya lango la Coastal lakini Ngoma anazuiwa na mabeki Coastal wanaondosha

(KULE MWADUI COMPLEX, AZAM FC INAONGOZA KWA BAO 1-0)
Dk 29, Mohammed anapata nafasi nzuri kabisa katika lango la Yanga lakini Yondani anafanya vema na Dida anaondosha mpira
Dk 23, Hamad Juma tena, anapiga shuti lakini Kamusoko anamwahi na kuzuia
Dk 20 Coastal wanapata kona ya pili, inapigwa lakini haina madhara
Dk 16, Hamad Juma anapoteza nafasi nzuri kabisa lakini Cannavaro anauwahi mpira na kuokoa
Dk 6 hadi 11, Coastal Union wanaonekana kuchangamka na kuwashambulia sana Yanga ambao wanaonekana kuwa makini kwenye ulinzi
Dk 4, Hamadi Juma anaingia vizuri lakini Yanga wanaokoa na kuwa kona ya kwanza ya mchezo. Inapigwa lakini haina madhara
Dk 3, Yusuf Sabo anaongia vizuri na kuangushwa lakini mwamuzi anasema twende
Mechi imeanza, kila upande unaonekana kuwa makini na kucheza taratibu kumsoma mwenzake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV