April 24, 2016


Nguli wa muziki wa Kikongo, Papa Wemba ambaye anajulikana kwa majina mengi yakiwemo King of Rhumba Rock, amefariki dunia baada ya kuanguka jukwaani wakati alipokuwa akitumbuiza jijini Abidjan nchini Ivory Coast. 


Papa Wemba ni mmoja wa wanamuziki waliochangia kukua kwa muziki wa Afrika na pia wanamuziki wengi wakubwa wamepita mikononi mwake.

Mpaka mauti yanamkuta alikuwa na umri wa miaka 66, video ya tukio inaonyesha alianguka ghafla wakati wacheza shoo wake wakiwa mbele ya jukwaa na waliendelea kucheza kwa hatua kadhaa kabla ya kusitisha na kwenda kumuangalia akiwa chini.

Inaelezwa kuwa tukio la kuangula lilitokea mara baada ya Papa Wemba kuimba wimbo wake wa tatu jukwaani hapo.
 Kituo cha redio cha Okapi cha DR Congo kilitangaza juu ya kifo hicho lakini sababu hasa haijatajwa.

Marehemu ambaye jjina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba alikuwa kitumbuiza kwenye Tamasha la ‘Urban Music Festival’

Papa Wemba
Kuzaliwa: Juni 14, 1949
Kufariki: Aprili 24, 2016
Aina ya muziki aliokuwa akiimba: Soukous, Rhumba


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic