April 23, 2016Mashabiki wa timu ya Coastal Union wameandaa wimbo maalum kwa ajili ya Yanga lakini watakuwa wakiimba kwa lugha ya Kiarabu.

Yanga watakuwa wageni wa Coastal Union katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, kesho.

Coastal Union imeingia nusu fainali baada ya kuitwanga Simba kwa mabao 2-1 katika hatua ya robo fainali.
Mashabiki hao, wameamua kutumia wimbo wa Kiarabu kwa jina la “Helua Helua”, ili kuwachanganya Yanga.

Said Salim, mmoja wa mashabiki wa Coastal Union ameiambia SALEHJEMBE, kwamba watakuwa wakifanya hivyo ili kuwaonyesha kweli wao ni Waarabu wa Tanga.


“Wanatuita Waarabu wa Tanga, sasa wanakuja kuchukua zao tatu hapa. Tutaendelea kupambana, kwamba tunafunga wao, wakati tunasubiri fainali, tunawamaliza huku jirani zetu na kubaki ligi kuu,” alisema.

Helua ni neno lenye maana ya kitu kizuri, kinachovutia au kufurahisha. Limekuwa maarufu sana baada ya mashabiki kusikia mtangazaji wa runinga ya Misri akitumia neno hilo baada ya Al Ahly kupata bao la pili dakika ya 90 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuing'oa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV