April 23, 2016


Na Saleh Ally
Shabiki mmoja wa Mwadui FC, maarufu kama “Matope” ameonekana kwenye runinga ya Azam TV akijisifia kuwa kesho  katika mechi ya Kombe la Shirikisho, watawamaliza Azam FC.

Azam FC watakuwa wageni wa Mwadui FC katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa Mwadui mkoani Shinyanga.


Azam TV ilitoa nafasi kwa mashabiki wa timu zote nne, yaani Yanga, Azam FC, Mwadui FC kujitapa.

Lakini shabiki huyo, alitumia muda mwingi kuelezea kuhusiana na mapanga aliyo nayo na atakavyowamaliza wenzake wa Azam FC.

Inawezekana ni utani, lakini kila mmoja anajua hakuna utani kwenye silaha. Hivyo lazima viongozi wawe makini na hilo.

Kama ataingia kajipaka matope, ni jambo la kawaida. Lakini kumruhusu aingie na mapanga kwa kisingizio ni staili yake ni kosa kubwa na hilo haliruhusiwi katika soka kwa kuwa mchezo huo si uadui.


Soka inakwenda na jazba kama ambavyo binadamu anavyoishi na ajali au majanga. Ni jambo usilolijua litatokea wakati gani.

Inawezekana kabisa Matope anaweza asilitumie panga yeye, lakini akatokea mtu akampokonya na kumdhuru mwingine.
Hivyo, TFF wanapaswa kulichukulia hilo kwa msisitizo wa juu. Kwamba kesho uwanjani Matope aingie yeye mapenga yabaki nje au akiamua, abaki nayo yeye nje.


1 COMMENTS:

  1. Sasa wanaohusika na ulinzi na usalama wa mashabiki ni tff au jeshi la polisi?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV