MAUGO AKIWA CHINI BAADA YA KUANGUSHWA NA MBABE |
Baada ya kuchezea kichapo cha TKO ya raundi ya tatu, bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo amesema kipigo hicho kimetokana na purukushani za mpinzani wake, Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ kumtonesha majeraha ya nyonga aliyopata kabla ya pambano hilo.
Awali, Maugo alitamba kumuua Mbabe ili aweke heshima mjini, lakini mambo yakageuka na kujikuta akishindwa kuendelea na raundi ya nne ya pambano hilo la ubingwa wa Afrika UBO kilo 79 lililopigwa wikiendi iliopita kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar kufuatia kuangushwa mara tatu ndani ya raundi tatu hali iliyomfanya asalimu amri.
Maugo amesema sababu kubwa iliyomfanya ashindwe kuendelea na pambano hilo ni baada ya kujitonesha majeraha ya nyonga kufuatia uchezaji wa hovyo wa mpinzani wake.
“Unajua tatizo lililonifanya nishindwe kuendelea na pambano ni kwa sababu mpinzani wangu alikuwa anacheza hovyo sana na hajui kupangilia ngumi, amesababisha nitoneshe majeraha yangu ya nyonga niliyopata siku chache mazoezini.
“Nadhani kama nisingepanda ulingoni ungetokea utata mkubwa kwani hata kocha na meneja wangu nilishawaambia kuwa sitaweza kucheza na nilicheza kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki wangu tu kwani nilijua hata raundi ya kwanza na ya pili nisingemaliza, lakini nikafika hadi raundi ya tatu na kukubali wampe ushindi wa TKO,” alisema Maugo.
0 COMMENTS:
Post a Comment