April 25, 2016


Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja, amewaambia wachezaji wake kwamba hakuna mchezaji yeyote anayeidai klabu hiyo kwa kuwa kila mmoja amelipwa mshahara na posho, hivyo wanatakiwa kuchapa kazi wapeleke ubingwa Msimbazi.

Simba ipo visiwani Zanzibar ambako imeweka kambi ya muda mfupi kabla ya kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara huku ikiwa bado haijakata tamaa ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Wekundu wamebakiza nafasi moja tu ya ubingwa wa ligi ili kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao kufuatia kutupwa nje ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Mayanja alisema bado wana matumaini ya kutwaa ubingwa lakini kinachotakiwa ni kushinda mechi zao zote zilizobaki.

“Tutajipanga vyema kuhakikisha tunafanikiwa kutwaa ubingwa kwani kwenye mpira lolote linaweza kutokea, wachezaji wanatakiwa kujitambua na kujua jukumu lililopo mbele yetu kwa kila mtu kuonyesha morali kwani hakuna mchezaji yeyote hadi sasa anayedai mshahara wala posho, hivyo ni vyema wakajituma.

“Na iwapo hatutapata ubingwa msimu huu, basi hakuna haja ya mashabiki kukasirika na kukata tamaa, naamini kikosi hiki tukikijenga vyema na kuanza nacho msimu ujao, basi tutakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu ujao.

“Naomba msamaha kwa mashabiki, watulie, kwani kama tutajipanga vyema tutachukua ubingwa, kilichotokea ni kutokana na mipango yangu kuharibiwa na majeruhi ambao walikuwa katika mipango ya kikosi changu na kushindwa kucheza katika mechi mbili zililizopita,” alisema Mayanja.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic