April 17, 2016



Kocha Jackson Mayanga ana imani na maandalizi ya kikosi chake kuwa kina uwezo mkubwa kuwa kitaishinda Toto African kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

Hata hivyo, Mayanja anajua mechi yao hiyo ya leo itakuwa ni ngumu kwa kuwa Toto wangependa kushinda pia.

Katika mechi ya mzunguko wa timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba huku Toto wakisawazisha bao katika dakika ya mwisho kabisa.

Mayanja amesema wamejiandaa vizuri na kinachotakiwa ni kucheza kwa umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na kutumia nafasi.

"Kwenye mpira ukiwa makini unafanikiwa, ukikosea ujue utaadhibiwa. Sisi tumejiandaa vizuri na tunataka kucheza vizuri na kushinda.

"Wachezaji wangu wanataka kushinda, hivyo litakuwa ni jambo zuri tukiingia na kupambana kwa asilimia mia tukiwa makini," alisema.

Simba inarudi uwanjani leo katika mechi ya Ligi Kuu Bara baada ya kupoteza mechi yake ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Coastal Union. Ilifungwa mabao 2-1 na kung'olewa katika hatua ya robo fainali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic