April 17, 2016



Na Saleh Ally
Mambo ya utani si jambo baya sana. Picha hii imesambaa mtandaoni, kwamba Msemaji wa Yanga, Jerry Muro anajiandaa kwenda Misri wakati Msemaji wa Simba, Haji Manara yuko njiani kwenda Uwanja wa Taifa ambako timu yake inacheza na Toto African katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Picha hii inaonyesha namna watani Yanga na Simba wanavyoweza kutaniana. Ndege inayoonekana amepanda Muro haiwezi kutumika kwenda Misri, huenda walikuwa wanakwenda Pemba wakati ule walipoweka kambi. 

Lakini Manara pia ana haki ya kupanda bodaboda, kwanza kumbuka ana usafiri wake yaani gari. Lakini bado kutaniana si jambo baya lakini kuwa na staha.

Kuna ambao wamekuwa wakisambaza maneno mitandaoni, mengine ni dhihaka kuu kwa Manara, hilo si jambo jema.

BLOG YA SALEHJEMBE, inaweka msisitizo kwamba pamoja na tofauti ya timu tunazoshangilia, lakini hiyo haiwezi kuondoa utu na upendo miongoni mwetu.

Kila mtu aheshimu upenzi wa mwenzake, pia ni vizuri kuheshimu utu wa mtu maana ndiyo unaotufanya wote kuwa watu. Kama unaona maneno fulani ni dhihaka inayoingia kwenye mwili wa binadamu kama kashfa, vizuri kuiepuka. 

Lakini kama hii ya ndege na pikipiki, ni sehemu ya utani wa kawaida ambao si dhalili badala yake inaonekana watu wameunga ili kutaniana. Raha ya utani kucheka si kudhalilishana na kuudhiana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic