April 29, 2016Timu ya Mgambo ambayo juzi Jumatano ilipoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwa kufungwa mabao 2-1, imekuwa na rekodi ya aina yake tangu kwa mara ya kwanza ipande kucheza ligi kuu misimu minne iliyopita.

Mgambo ilipanda ligi kuu msimu wa 2012/13 ambapo kwa misimu yote hiyo haikuwahi kushuka daraja, lakini cha kushangaza ni kuwa imefanikiwa kufunga mabao mawili tu ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar kwa kipindi hicho chote.

Awali, timu hiyo ilicheza misimu mitatu mfululizo bila ya kuzifumania nyavu za uwanja huo, mpaka walipokuja kuvunja mwiko huo msimu huu walipocheza na Simba Februari 3, 2016 na kukubali kichapo cha mabao 5-1.


Straika wao hatari, Fully Maganga, ndiye aliyefunga dhidi ya Simba na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga bao kwenye Uwanja wa Taifa, pia juzi Jumatano, Bolly Shaibu Ajally alifanikiwa kufunga bao dhidi ya Yanga likiwa ni la pili kwa timu hiyo ndani ya misimu minne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV