April 9, 2016Mwananamuziki maarufu wa dansi nchini, Ndanda Kosovo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Taarifa zinazotufikia, zinaeleza Ndanda amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa tumbo.

“Alikuwa akiumwa tumbo na inaonekana kuna mishipa ilipasuka kwa ndani, ndiyo hivyo ametutoka,” alisema King Dodo.

Tumeelezwa mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Ndanda aliyekuwa maarufu kama "Kichaa" au Mjelajela" alitamba akiwa na bendi ya FM hasa baada ya wanamuziki wake kuswekwa lupango kutokana na kukosa kibao cha kuishi nchini.

Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV