April 16, 2016


Na Saleh Ally
DROO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua nusu fainali imepangwa, kila mtu ana mawazo yake, lakini ukweli mwisho anatakiwa kupatikana bingwa atakayetokana na timu mbili zitakazocheza nusu fainali.

Timu hizo zitapatikana kupitia mechi nne za nusu fainali ambazo zitaanza kuchezwa kuanzia Aprili 26 na 27 na kurudiana Mei 3 na 4, mwaka huu.

Katika timu zote nne zilizoingia nusu fainali, Man City itacheza dhidi ya Real Madrid wakati Atletico Madrid itaanzia nyumbani dhidi ya wababe wengine wa michuano hiyo, Bayern Munich, hakuna mechi laini wala rahisi, zote mtiti kweli.

MAN CITY Vs REAL MADRID:
Mechi hii itasikika zaidi kwa kuwa Real Madrid, timu kubwa zaidi katika zinazofika nusu fainali, inakutana na timu kutoka England, wanajulikana kwa kelele.

Wengi wanatoa nafasi kwa Madrid ingawa wanapaswa kuangalia namna ambavyo Man City imevuka, haikuwa timu laini.

Katika mechi kumi, imeshinda sita, sare mbili na kupoteza mbili wakati Madrid wameshinda nane, sare moja na kupoteza moja.

Kitakwimu, Madrid wako juu lakini Man City si wa kubeza hata kidogo na wana nafasi ya kuimarika baada ya kuingia hatua ambayo hawakutarajiwa.

Huenda Madrid watakuwa makini zaidi baada ya kipigo cha Wolfsburg na wakalazimika kutumia nguvu kubwa hatua ya robo fainali mechi ya marudio.

Itakuwa mechi ya burudani, itakuwa mechi ya timu na wachezaji mmojammoja, mfano Cristiano Ronaldo na Gareth Bale lakini Man City wana Sergio Aguero, Yaya Toure na wengine. Hivyo ufundi utatawala lakini kasi na kutaka ushindi itakuwa nguzo.


Manchester City
P10 W6 D2 L2
Makundi: *Ilishika nafasi ya 1- (Juventus, Sevilla, Monchengladbach)
16 Bora: bt Dynamo Kiev (3-1, 0-0)
Robo: iliwafunga Paris Saint-Germain (2-2, 1-0)

Real Madrid
P10 W8 D1 L1
Makundi: *Ilishika nafasi ya 1-(Paris Saint-Germain, Shakhtar Donetsk, Malmo)
16 Bora: Waliishinda Roma (2-0, 2-0)
Robo: Waliitoa Wolfsburg (0-2, 3-0)

WAFUNGAJI MSIMU HUU:
Manchester City
Kevin De Bruyne – mechi 8, mabao 3
Raheem Sterling – mechi 8, mabao 3
Wilfried Bony – mechi 5, mabao 2
Sergio Agüero – mechi 7, mabao 2
David Silva – mechi 7, mabao 2


Real Madrid
Cristiano Ronaldo – mechi 10, mabao 16
Karim Benzema – mechi 7, mabao 4
Jesé – mechi 7, bao 1
James Rodríguez – mechi 4, bao 1
Mateo Kovacic – mechi 7, bao 1

ATLETICO VS BAYERN:
Atletico Madrid na Bayern Munich kwa mara ya mwisho zilikutana Mei 17, 1974 katika mechi ya Kombe la Ulaya. Safari hii zinakutana katika mashindano ya juu kabisa katika soka barani Ulaya.

Katika msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu hizi, kila moja inaonekana ina nafasi ya kutwaa ubingwa, hilo halitakuwa jambo la ajabu.

Tangu  hatua ya awali, zilionyesha ni zile timu zitakazofika mbali. Kila moja ikashika nafasi ya kwanza katika kundi lake.

Katika mechi 10, Bayern imeshinda saba, sare mbili na kupoteza moja wakati Atletico imeshinda tano, sare tatu na kupoteza mbili. Katika hatua hii, Bayern wako juu zaidi.

Katika hatua ya mtoano hasa robo fainali, Atletico wamekuwa hatari baada ya kumvua ubingwa Barcelona wakati Bayern waliimaliza Benfica ya Ureno.

Makocha wanaokutana ni Pep Guardiola atakayekuwa akipambana na staili ngumu na imara ya ulinzi ya Diego Simeone.

Aina yake ya ukabaji ni imara zaidi huenda kuliko timu zote zilizoingia nusu fainali na anatumia mashambulizi ya kushitukiza. Ingawa safu ya Bayern pia ni hatari kwa ‘counter attack’.

Mechi hii inaweza kuwa ngumu zaidi hatua hii, bado mshindi wa hapa anapewa nafasi ya kuwa bingwa kwa asilimia 54.

WALIVYOFIKA NUSU FAINALI:

Atletico
P10 W5 D3 L2
Makundi: *Ilishika nafasi ya 1- (Benfica, Galatasaray, Astana)
16 Bora: iliwafunga PSV Eindhoven (0-0, 0-0; 8-7 kwa penalti)
Robo: Waliitoa Barcelona (1-2, 2-0)


Bayern
P10 W7 D2 L1
Makundi: *Ilishika nafasi ya 1- (Arsenal, Olympiakos, Dinamo Zagreb)
16 Bora: Waliitoa Juventus (2-2, 4-2 aet)
Robo: Waliitoa Benfica (1-0, 2-2)

WAFUNGAJI BORA
Atletico
Antoine Griezmann – mechi 10, mabao 6
Saul Niguez – mechi10, mabao 2
Ángel Correa - mechi 5, bao1

Bayern
Robert Lewandowski – mechi 10, mabao 8
Thomas Müller  - mechi 10, mabao 8

Arjen Robben – mechi 3, mabao 2


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic