Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwenye jiji la Dar es Salaam zimesababisha hofu ya kuahirishwa kwa mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar inayosubiriwa kwa hamu kubwa.
Iwapo Yanga itashinda katika mechi ya leo, basi moja kwa moja itakwea kileleni mwa Ligi Kuu Bara.
Lakini tayari Yanga wameweka msisitizo kwamba wana matumaini ya asilimia 100 hadi sasa mechi hiyo itakuwepo.
Kwa upande wa TFF, msemaji wake, Baraka Kizuguto amesema mechi itakuwepo kwa kuwa mvua zinanyesha na kukatika.
“Mvua za mfululizo zilikuwepo tokea asubuhi lakini sasa matumaini yanaonekana kwamba zimekatika.
“Hivyo hakuna sababu ya mechi hiyo kuahirishwa na watu wengu mitandaoni wamekuwa na hofu hiyo lakini mvua zimekatika sasa, mashabiki wajisogeze tu tujumuike pamoja huku,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment