April 21, 2016

Matajiri wa Hispania, Real Madrid wanapanga kumuongezea mkataba wa miaka minne fowadi wake, Cristiano Ronaldo na kukata mzizi wa fitina juu ya hatima yake hapo baadaye.

Tangu mwanzoni mwa msimu huu, rais wa klabu hiyo,  Florentino Perez alikuwa na mpango wa kumuachia staa huyo ajiunge na miamba ya Ufaransa, PSG kwa kitita kilichokadiriwa kufikia euro milioni 100.

Hata hivyo kitendo cha Ronaldo kufunga mabao zaidi ya 30 kwa msimu sita mfululizo huku Gareth Bale kipenzi cha Perez ambaye alitaka awe mbadala wa Ronaldo ameshindwa kuonyesha kiwango pamoja na kuandamwa na majeruhi.

Licha ya ofa hiyo, huenda kusiwe na mabadiliko katika mshahara wake wa euro milioni 21 kwa mwaka anazopokea kwa sasa, zaidi Madrid imenogewa kuendelea naye.

Aidha, kiungo mshambuluaji James Rodriguez na Isco ndiyo wana nafasi kubwa ya kuondoka kwenye majira ya kiangazi.

TAKWIMU ZA RONALDO 2015-16

La Liga 
Mechi 34, mabao 31, asisti 11
Ligi ya Mabingwa
Mechi 10, mabao 16, asisti 4 0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV