April 21, 2016



Baada ya Yanga kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly ya Misri na hivyo kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, timu hiyo ya Jangwani sasa inajiandaa kucheza katika Kombe la Shirikisho.


Kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) zinaeleza kuwa timu ambazo zitatolewa katika Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika zitashuka katika Kombe la Shirikisho ambapo huko zitakutana na timu nane zilizosonga mbele ambapo zitacheza mechi za mtoano za nyumbani na ugenini kisha zitakazofuzu zitaingia hatua ya makundi.


 
Baada ya Yanga kutolewa, sasa inasubiri ratiba kujua timu ambayo itapangwa nayo katika mechi hizo mbili za mtoano za nyumbani na ugenini ambazo zitachezwa wiki ya Mei  6-8, mwaka huu na marudio ni Mei 17-18, 2016.


Timu ambazo Yanga inatarajiwa kukutana na moja wapo ni hizi hapa huku timu kutoka nchi za Kiarabu zikiwa zimetawala hivyo kuwa na uwezekano wa kurudi kwa Waarabu kama ilivyokuwa kwa Al Ahly ya Misri. 


Sagrada Esperança - Angola
Misr El-Makasa - Misri
CF Mounana - Gabon
Medeama - Ghana
FUS Rabat - Morocco
Kawkab Marrakech - Morocco
Espérance de Tunis - Tunisia
Stade Gabèsien - Tunisia

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic