April 18, 2016

Mayanja

RAIS wa Simba, Evans Aveva, amesema wanasubiria ripoti ya kocha Mganda, Jackson Mayanja ili kujua iwapo watamuongeza mkataba au la.

Mayanja alipewa mkataba wa muda mfupi  wa kuinoa Simba ambao unatarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuondoka kwa Muingereza Dylan Kerr.

Hata hivyo, Mayanja alieleza kuwa, kuna timu kadhaa zinamfuatilia za hapa Tanzania na nje ya Tanzania na kudai kuwa yupo kikazi na anakaribisha mazungumzo na timu yoyote, japokuwa anaipa nafasi ya kwanza Simba.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Aveva alisema  wanasubiri ligi ifikie tamati ili waweze kukaa chini na Mayanja kuzungumza ili kujua iwapo watamuongeza mkataba mwingine au la.

Aveva

“Tunasubiria ligi itakapofikia tamati ndiyo tuweze kukaa naye chini kwa kuangalia ripoti yake inasemaje ndipo tuamue la kufanya. Lakini tunajua kocha anaweza kuwa na mipango yake, hivyo kila kitu kitajulikana huko mbele baada ya ligi kuisha.

“Kuhusu kuwa na mipango ya kuwa na kocha mwingine, bado haijajulikana na siwezi kusema chochote, kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye ligi,” alisema Aveva.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic