April 23, 2016


Nahodha na mshambuliaji nyota wa Manchester United, Wayne Rooney ndiye mwanamichezo tajiri zaidi wa Uingereza kwa kipindi hiki.

Kwa mujibu wa list ya wanamichezo matajiri 2016 iliyotolewa na gazeti la Sunday, Rooney ndiye anayeshika mamba moja Waingereza.

Lakini Rooney ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwa wale waliopo Ligi Kuu England.

Imeelezwa Rooney ana utajiri wa pauni million 82 kwa mwaka ambao unatokana na kipato chake katika mshahara wake mkubwa anaolipwa na Manchester United. Anapokea pauni 300,000 kwa wiki.

Ukiachana na mshahara, pia Rooney ana mikataba minono kupitia kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike pamoja na ile ya vifaa vya umeme ya Samsung.

Hii inamfanya awe juu ya wachezaji wengi akiwemo Bale ambaye ni mchezaji ghali duniani anayekipiga Real Madrid.


Uingereza inajumuisha England, Scotland pamoja na Wales anapotokea Bale ambaye anaingiza pauni milioni 34.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV