April 23, 2016

STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe amejisikitikia kwa kushindwa kuonyesha uwezo wa juu katika michuano ya kimataifa anapokuwa na timu yake tofauti na anavyofanya katika Ligi Kuu Bara.

Katika ligi kuu Tambwe ana mabao 18 akiwa amezidiwa moja na Hamis Kiiza wa Simba, lakini kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, straika huyo amefunga bao moja tu.

Tambwe amekuwa akianzia benchi au akifanyiwa mabadiliko katika michezo ya hivi karibuni ya Yanga kutokana na kushindwa kuonyesha uwezo wa kuridhisha.

Akizungumzia hali hiyo, Tambwe aliliambia Championi Jumamosi: “Hata mimi najishangaa kwa nini nimekuwa hivyo kwani nafanya vizuri mazoezini lakini pia katika ligi kuu.

“Sina jinsi lakini nitaongeza jitihada mazoezini ili nirudi kwenye kiwango changu cha siku zote. Najua mashabiki wanataka kuniona nikiwa sawa, nitaongeza jitihada niwe fiti.”

Katika mechi sita za Yanga za Ligi ya Mabingwa Afrika, timu hiyo imefunga mabao tisa ambapo matatu kati ya hayo amefunga Donald Ngoma.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV