April 15, 2016

JUUKO
Simba inashuka dimbani Jumamosi kuwavaa Toto African ya Mwanza. Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, lakini itamkosa beki kisiki, Juuko Murshid.

Juuko raia wa Uganda ana kadi tatu za njano, hali itakayomlazimu Kocha Jackson Mayanja kufanya mipango mingine.

Mayanja alisema wachezaji wengine watakaoukosa mchezo huo ni Mwinyi Kazimoto, Brian Majwega ambao wote ni wagonjwa huku kipa Vincent Angban na kiungo Justice Majabvi wakiwa kwenye hatihati ya kutocheza kutokana na kukosa mazoezi ya jana kwenye Uwanja wa Ndege Beach, Mbweni.

“Kumkosa Juuko ni pengo lakini hakuna jinsi, tutaangalia wengine waliopo,” alisema kocha huyo wa zamani wa Vipers na Kagera Sugar.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV