Kiwango cha uchezaji cha mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga, kinaonyesha kutowafurahisha mashabiki wa Yanga. Wanaona ameshuka, huenda amechoka na anastahili kupumzishwa.
Tambwe mwenye mabao 18 katika Ligi Kuu Bara ameshindwa kufunga na hata kiwango chake kimeonekana kuwa cha chini.
Baada ya mechi hiyo dhidi ya Mwadui FC, mashabiki kadhaa walimtaka kocha Hans van der Pluijm kutompanga Tambwe katika mechi zijazo na nafasi yake ichukuliwe na Malimi Busungu kwa madai kuwa hivi sasa anawazingua.
Hata hivyo, Pluijm alichukizwa na kauli hizo na ndipo alipoanza kuzozozana nao mpaka askari walipoingilia kati na kumtaka kocha apande gari aondoke uwanjani hapo.
Pamoja na hivyo, katika mazungumzo ya awali na gazeti hili kabla ya tukio hilo, Pluijm alionyesha kusikitishwa na kiwango alichoonyesha Tambwe.
“Sijui ni kwanini ila nitakaa na washambuliaji wangu waniambie wana matatizo gani kwani siyo kawaida yao,” alisema Pluijm ambaye pia alisema haridhishwi na kiwango cha sasa cha mshambuliaji wake mwingine, Donald Ngoma.
0 COMMENTS:
Post a Comment