MPIRA UMEMALIZIKA, SIMBA WAMEFUNGWA BAO 1-0.
Dakika ya 93+
Dakika ya 92+
Zimeongezwa dakika 4 za muda wa nyongeza.
Dakika ya 90
Dakika ya 89: Nimubona anapiga krosi, kipa wa Toto anaruka anaikosa, anagongana na Lyanga, mchezo umesimama kwa muda kipa anatibiwa.
Dakika ya 88: Toto wanapiga kona inaokolewa.
Dakika ya 88: Toto wanapata kona
Dakika ya 87: Simba wanaendelea kupambana lakini Toto wanakuwa wazuri wa kumiliki mpira.
Dakika ya 84: Kiiza anapiga shuti linadakwa na kipa wa Toto.
Dakika ya 82: Toto wanafanya mabadiliko, anatoka Jafar Mohamed, anaingia William Kimanzi.
Dakika ya 80: Matokeo bado 0-1
Dakika ya 79: Ajib anachukua mpira vizuri anatoa pasi ya kisigino kwa Mkude ambaye anapiga shuti linapaa juu ya lango la Toto.
Dakika ya 75: Ibrahim Ajib anapewa kadi ya njano kwa kumfokea mwamuzi wa pembeni.
Dakika ya 72: Toto wanafanya mabadiliko, anatoka Edward Christopher anaingia Japhet Vedastus.
Dakika ya 71: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Kessy ametolewa nje kwa kadi nyekundu. |
Dakika ya 65: Toto wanacheza kwa kujiamini kutokana na Simba kuwa pungufu.
Dakika ya 58: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mwalyanzi anaingia Ibrahim Ajib.
Dakika ya 56: Toto wanafanya mabadiliko, anatoka Jama Soud anaingia Salimin Hozza.
Dakika ya 50: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mgosi anaingia Nimubona.
Dakika ya 49: Mohammed Hussein wa Simaba napiga shuti linapiga nyavu ndogo na kutoka nje.
Dakika ya 47: beki wa Simba, Hassan Kessy anapewa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo, Edward Christopha wa Titit, analalamika lakini wenzake wanamtoa nje.
Kipindi cha pili kimeanza
Dakika 45: Zimekamilika, sasa ni mapumziko.
Dakika ya 45+: Beki wa Toto, Yusuph Mlipili anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Kiiza.
Dakika 3 za nyongeza
Dakika ya 45: Kessy anapiga krosi nzuri lakini washambuliaji wa Simba wanashindwa kuitumia vizuri.
Dakika ya 40: Matokeo bado ni Simba 0, Toto 1, mashambulizi ni ya kupokezana.
Dakika ya 38: Simba wanashambulia lango la Toto lakini Toto nao wanajibu mashambulizi.
Baada ya Mayanja kutolewa, Kocha wa Makipa wa Simba, Adam Abdallah ndiye ameshika majukumu ya kuiongoza timu.
Mayanja ameondolewa kwenye benchi na mwamuzi Ahmada kutokana na kinachoonekana wamepishana kauli.
Dakika ya 31: Kocha wa Simba analalamika kwa mwamuzi, mwamuzi anamtoa nje Kocha Mayanja.
Kocha Mayanja |
Dakika ya 3: Lyanga anafanyiwa faulo, Simba wanapata faulo.
Dakika ya 29: Mchezo umechangamka, Simba wanafanya mashambulizi kutafuta bao la kusawazisha.
Dakika ya 27: Awadhi Juma anakosa bao la wazi, anapata pasi kutoka kwa Lyanga, anaupiga kwa kichwa unatoa kidogo nje ya lango la Toto.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!
Dakika ya 23: Toto wanaongoza bao 1-0, Simba waliuanza mchezo kwa kasi ndogo, sasa wanaonekana kuanza kuchangamka.
Dakika ya 20: Toto wanapata bao, mfungaji akiwa ni Wazir Junior baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 likajaa wazuni moja kwa moja.
Dakika ya 19: Simba wanapata faulo nje ya 18 ya Toto upande wa kulia mwa uwanja, Kessy anapiga lakini kipa wa Toto anadaka na kuupiga mbele.
Dakika ya 16, matokeo bado 0-0, timu zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 12: Awadhi Juma anapiga shuti kali lakini linatoka nje.
Dakika ya 10: Toto wanapiga faulo lakini inapaa juu ya lango la Simba na kuwa goal kick.
Dakika ya 9 Toto wanapata faulo nje ya 18 ya Simba.
Dakika ya 8: Simba wanamiliki mpira muda mwingi ila bado hawajatengeneza nafasi.
Dakika ya 5: Timu zote bado zinasomana taratibu, mchezo haujawa na kasi kwa timu zote.
Dakika ya kwanza: Mchezo umeanza.
Mchezo utaanza muda wowote kuanzia sasa
KIKOSI CHA SIMBA
Vincent Angban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novat Lufunga, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Peter Mwalianzi, Awadh Juma, Daniel Lyanga, Hamis Kiiza na Musa Mgosi
Walio benchi:
Manyika Peter, Said Issa, Moahmmed Fakhi, Said Ndemla, Emery Nimubona, Paul Kiongera na Ibrahim Ajib
KIKOSI CHA TOTO AFRICANS
Mussa Kirungi, Erick Mlilo, Salum Chukwu, Yusuph Mlipili, Hassan Khatibu, Carlos Protas, Jama Soudy, Abdallah Seseme, Wazir Junior, Edward Christopher na Jafari Mohammed.
Walio benchi
Faustin Msafiri, Miraji Makka, Salmin Hozza, Ladislaus Mbogo, William Kimanzi, Jackson Dickson na Japhert Vedastus.
Timu ndiyo zinaingia uwanjani hapa Taifa.
Mashabiki wa Simba. |
Timu zinapasha misuli uwanjani muda huu
Mchezo wa Ligi Kuu Bara, Simba inashika nafasi ya pili katika msomamo ikiwa na pointi 57, nyuma ya Yanga yenye pointi 59 zote zikiwa zimecheza mechi 24. Toto yenyewe inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 27katika michezo 26 iliyocheza mpaka sasa.
Haya sasa semeni,hao ni wamchangani tuu hata iweje!
ReplyDelete