April 28, 2016


Simba imecheza mechi ya kirafiki na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mafunzo huku kiungo wake Awadhi Juma akionyesha uhai kwa kufunga mabao yote matatu, yaani hat trick.

Awadhi amefunga mabao hayo katika mechi hiyo ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo.

Simba imeweka kambi Zanzibar kujiandaa na mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC, keshokutwa Jumapili.

Mechi hiyo ilianza taratibu huku Mafunzo wakiupoozesha mpira kabla ya kulazimishwa kuchangamka baada ya kuwaona Simba wakishambulia mfululizo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV