April 14, 2016


Hakuna refu lisilokuwa na ncha. Mcheza kikapu maarufu wa Marekani, Kobe Bryant amestaafu.

Nyota huyo wa LA Lakers amestaafu na kuagwa na mashabiki kibao wakiwemo nyota wa muziki kama Jay Z, soka wakiongozwa na David Beckham na kikapu wakiongozwa na Magic Johnson.

Katika siku ya kuagwa, Kobe aliyecheza kwenye NBA kwa miaka 20 aliingoza Lakers kushinda kwa pointi 101-96 dhidi ya Utah Jazz huku yeye akifunga pointi 60 na kuweka rekodi ya aina yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV