April 14, 2016
Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo amesema Yanga na Azam FC wamezoea kudekezwa.

Julio amesema Yanga na Azam FC wanataka mechi zao za nusu fainali ya Kombe la Shirikisho zisogezwe mbele kwa kuwa wana tabia za kudeka na hawataki wengine wawe mabingwa.

Yanga imepangiwa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani na Azam FC wanatakiwa kuifuata Mwadui FC kwenye mji wa madini wa Shinyanga. Mechi hizo zote zinatakiwa kupigwa Aprili 24.

Lakini tayari Azam na Yanga wamesema wanaomba kusogezwa mbele kwa kuwa ndiyo watakuwa wamerudi kutoka Misri na Tunisia wanaposhiriki michuano ya Kombe la Shirikisho na  Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Wanarudi tarehe 21, baada ya hapo siku inayofuata ambayo ni tarehe 22 wanapanda ndege ya saa moja tu kwenda kwenye kituo,” alisema Julio.

“Tatizo lao ni lipi, hofu yao ni ipi? Au kwa kuwa hawapendi kuwaona wengine wanakuwa mabingwa. Waache hayo mambo yao, waje wacheze mpira na TFF waliangalie hilo,” alisema Julio.
2 COMMENTS:

  1. Sasa Julio Tanga kuna uwanja wa ndege wa kuruhusu ndege kubwa kutua hadi Yanga waende kwa ndege huko?Au ndio mfa maji haachi kutapatapa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Julio hana lolote, maneno mengi mpira hafifu. Sasa kama anajiamini kweli, mechi hzo zikisogezwa mbele zitamuathiri vp km kocha aliyeiandaa timu yake kutwaa ubingwa?

      Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV