April 10, 2016


Wachezaji wawili wenye miili midogo, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Farid Mussa wamekuwa waokozi wa Azam FC baada ya kila mmoja kufunga bao moja na kutoa pasi ya moja.

Singano na Farid, kila mmoja alifunga baada ya kupewa pasi na mwenzake wakati Azam FC ilipoichapa Esperance ya Tunisia kwa mabao 2-1 katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Tayari wakongwe John Bocco ambaye ni nahodha na mkongwe mwingine, Kipre Tchetche walishindwa kabisa kuonyesha cheche baada ya kupoteza zaidi ya nafasi nne za kufunga.


Cheki pichaaaz.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV