April 14, 2016


Umeona timu nne zilizovuka na kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kila moja ilishinda kwa jumla ya mabao 3-2.

Tuanza na Real Madrid, mechi ya kwanza ilifungwa kwa mabao 2-0 dhidi ya Wolfsburg ya Ujerumani. Mechi ya pili mjini Madrid ikashinda kwa mabao 3-0 na kufanya jumla iwe 3-2.

Atletico Madrid ikiwa ugenini, ikapoteza kwa mabao 2-1 lakini nyumbani, ikashinda kwa mabao 2-0. Jumla ikawa 3-2.

Manchester City ikiwa ugenini Paris, ikapambana na kupata sare ya mabao 2-2. Iliporejea England, ikashinda 1-0 dhidi ya PSG. Jumla ikawa mabao 3-2.

Bayern Munich wao walianza kushinda nyumbani kwa bao moja, lakini waliposafiri kwenda Ureno kuwafuata Benfica, matokeo yakawa sare ya 2-2. Jumla ni mabao 3-2, Bayern wakisonga mbele.

Itakuwaje kwenye hatua hiyo ngumu. Kwanza tusubiri droo itakayopangwa kesho, nani atacheza dhidi ya nani..

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV