April 28, 2016


Uongozi wa Coastal Union umesema haumpendi wala hautaki kumuona mwamuzi Abdallah Kambuzi kutoka Shinyanga.

Kambuzi alichezesha pambano la nusu fainali ya Kombe la FA kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, lakini pambano hilo likavunjika.

Katibu Mkuu wa Coastal Union, Salim Bawazir amesema mwamuzi huyo amekuwa 'akiwauma' na kusisitiza hata katika mechi yao dhidi ya Yanga ndiye aliyasababisha wao kuvuruga mchezo wao.

"Hakika haikuwa sawa hata kidogo, wametuonea na hatukubaliani na hili. Tunaamini kabisa hata kuwapa Yanga ushindi si maamuzi sahihi.

"Kama mwamuzi alishindwa kuumudu mchezo, vipi ushindi apewe Yanga. Kwanini mechi isirudiwe ili iwe fea game? Kamati ya utendaji itakutana na sisi tutalifanyia kazi.

"Kamati ya utendaji ikikaa, mwisho tutafikia makubaliano na kujua nini cha kufanya na baada ya hapo tutatoa kauli yetu," alisema Bawazir. 

Mechi hiyo ilivunjika huku Yanga ikiongoza kwa mabao 2-1, lakini bao la kwanza la Yanga alilofunga Donald Ngoma lilianizisha utata.

Lakini utata huo ukawa mkubwa zaidi baada ya Amissi Tambwe kufunga bao la pili akiusukumiza mpira kwa mkono.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic