April 24, 2016



Hauijulikani kama Yanga imesonga fainali ya Kombe la FA au itakuwa tofauti.

Mechi yake dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga imeisha ikiwa Yanga inaongoza kwa mabao 2-1. Lakini mwamuzi alimaliza baada ya kuzuka kwa tafrani na kipa wa Yanga Deogratius Munish ‘Dida’ kushambuliwa na mashabiki.

Pia beki Oscar Joshua akapigwa chupa kichwani. Mashabiki hao walionekana walikuwa wakipinga Yanga kupewa bao.

Amissi Tambwe aliyeingia kuchukua nafasi ya Donald Ngoma alifunga bao la pili kwa mkono.

Kabla ya hapo, Ngoma alifunga bao ambalo wachezaji wa Coastal Union walilalamika ni off Side.

Sasa haikujulikana mechi ilikuwa imeisha, au mwamuzi amemaliza kabla na suala hilo litakuwaje.

Lakini taratibu na kanuni zinaonyesha Yanga inaweza kupewa ushindi ikibainika mashabiki waliofanya vurugu ni wa Coastal Union lakini pia mchezo unaweza kuchezwa kwa dakika zilizobaki kama mashabiki waliofanya vurugu hawatakuwa wa Yanga au Coastal. 



7 COMMENTS:

  1. Sikutegemea mwandishi kama wewe upepese macho katika hili!! Uwanja ni wa coast kwahiyo ni wazi waliofanya fujo ni mashabiki wa coast na walikuwa na nia ya kuwadhuru wachezaji w Yanga. Mipira ya kihuni imepitwa na wakati ndo maana kila timu zetu zinapoenda nje zinalalamika kuonewa na marefa.

    ReplyDelete
  2. af Salehe unaandika eti".......baada ya yanga kupewa goli..." kweli...?
    nani kapewa goli....? mpira umegonga post ukarudi na kumgonga tambwe mkononi ni obviously ball to hand situation ambayo ni under the discretion of referee to make a call na any call atakayo fanya itakua sahihi.
    sasa upewaji uko wapi hapo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa kuna goli la mkono duniani mpaka useme mwamuzi hakuwapa goli imekuwa netball hiyo goli lolote la mkono la kupewa mpaka leo uingereza wanalishtaki goli la maradona

      Delete
    2. sasa wewe khalfani ujiulize mwenyewe hakuna goli la mkono kwahyo goli la yanga ni goli maana sio la mkono.
      alaf umetoa mfano wa goli la maradona situation zake ni tofauti kabisa kama hujui maradona alinyanyua mkono ukaenda kupiga mpira sasa tambwe alinyanyua mkono...? ni mpira umefuata mkono wa tambwe....
      kua makini

      Delete
  3. Nadhani kuna itajika darasa kidogo hiyo ilikuwa ball hand maana yake ni mpira umegonga mkono kwa hiyo ni sahihi kabisa goli, kama mkono kwa makusudi kabisa kashika mpira hiyo ni hand ball tafadhali kuwa makini na sheria za mpira si ushabiki tu. Asantani.

    ReplyDelete
  4. SISHABIKII YANGA WALA COASTAL UNION,LAKINI KWA KUFUATA SHERIA ZA MPIRA YANGA WANASTAHILI KUSONGA MBELE,HALAFU MASHABIKI WA COASTAL WASIINGIE TENA UWANJANI HATA KWENYE MECHI ZILIZOBAKI ZA VPL.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic