April 24, 2016


Azam FC imetinga fainali ya Kombe la FA baada ya kuishinda Mwadui FC kwa mikwaju ya penalti 5-3 katika mechi iliyocheza kwenye Uwanja wa Mwaduo Complex, Shinyanga.

Beki Aggrey Morris ndiye alifunga penalti ya mwisho iliyoifikisha Azam FC fainali hiyo.

Kabla ya mikwaju ya penalti, mechi hiyo iliisha kwa sare ya mabao 2-2 katika dakika 120 na baada ya hapo ikaamuliwa mikwaju ipigwe.

Bado haijajulikana kuhusiana na mchezo mwingine wa nusu fainali kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga ambao mwamuzi alivunja kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Yanga ilikuwa inaingoza kwa mabao 2-1, moja likifungwa na Donald Ngoma ambaye alionekana katika nafasi ya kuotea na la pili likafungwa na Amissi Tambwe ambaye alitumia mkono kuusukuma mpira wavuni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV