April 21, 2016


Na Saleh Ally, La Coruna
Washindi wa “Kwea Pipa Kwenda Spain na Azam Sports HD” wameweka rekodi kwa kuwa kati ya Watanzania waliopata nafasi ya kushuhudia maandalizi kabla ya moja ya mechi kubwa ya Ligi Kuu ya Hispania.

Washindi hao wameshuhudia maandalizi ya mechi kati ya wenyeji Derpotivo La Coruna kwenye Uwanja wao wa Raizor mjini hapa wakijiandaa kuivaa Barcelona.

Washindi Ismail Salim na Jamal Mussa walifika mapema uwanjani hapo wakiongozana na washindi kutoka Hong Kong na Sweden na kushudia mambo yanavyokwenda kabla ya kuanza mechi.

Pia waliendelea kutembezwa sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwekwa sehemu ambayo walipita wachezaji wa timu zote mbili wakiwemo Lionel Messi, Luis Suarez, Neymar na mastaa wengine.

Sehemu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya VIP tu na washindi hao wakawa karibu kabisa na wachezaji hao jambo ambalo lilikuwa faraja kubwa kwao.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV